The winning entry has been announced in this pair.There were 10 entries submitted in this pair during the submission phase, 4 of which were selected by peers to advance to the finals round. The winning entry was determined based on finals round voting by peers.Competition in this pair is now closed. |
Kauli mbiu katika karne hii angalau katika nchi zilizoendelea ni kwamba watu wanatamani kupata utulivu ila hawawezi kuupata. Kelele za magari barabarani, mikirizo isiyoisha ya simu, matangazo ya kidijitali ndani ya mabasi na magari ya moshi, Televisheni zinazowashwa hata katika ofisi ambapo watu hawapo, ni matatizo makubwa na vurugu isioisha. Binadamu wanajiangamiza wenyewe kwa kelele na wanatamani hali iwe tofauti-iwe porini, baharini au katika sehemu maalum zilizotengwa kwa ajili ya utulivu na umakinifu. Msomi wa historia, Alain Corbin anaandika akiwa mafichoni katika eneo la Sorbonne, naye Mtafiti kutoka Norwei, Erling Kagge kutoka katika kumbukumbu zake za the wastes of Antarctica, ambapo wote wamejaribu kutorokea. Na bado, anavyoeleza Bw. Corbin katika makala ya "A History of Silence", huenda sasa hakuna kelele tena kama ilivyokuwa hapo zamani. Kabla ya kuja kwa magurudumu ya magari ya kujazwa pumzi, barabara za jiji zilijawa na kelele za magurudumu za chuma na kelele za vyuma walivyovalishwa farasi wakikimbia kwenye mawe. Kabla ya kuja kwa simu za mkononi zilizosababisha watu kujitenga, mazungumzo yalishamiri ndani ya mabasi na magari ya moshi. Wauza magazeti hawakupanga bidhaa zao na kutulia tu ila walizitangaza kwa kupaza sauti sana na wauza matunda mbalimbali na samaki vilevile hawakuachwa nyumba. Sehemu za maonyesho ya sanaa zilijawa vifijo na nderemo za mashabiki kushangilia na kusuta. Hata katika maeneo ya mashambani, wakulima waliimba wakifanya kazi zao za sulubu. Siku hizi hawaimbi tena. Kilichobadilika sio hasa kiwango cha kelele, ambacho wanajamii katika miongo iliyopita pia walilalamikia ila ni kiwango cha vurugu ambacho kimechukua nafasi ambayo huenda ingechukuliwa na hali ya utulivu. Kunatokota hali ya kinaya tena kwa sababu iwapo utulivu utakuwepo-katika kina chake halisi, katika sehemu zenye upweke, katika chumba kilichohamwa ghafla-mara nyingi huwa ni hali isiyo ya faraja badala ya kuwa ya hali ya kukumbatiwa. Hali ya uwoga huingia; masikio yanamakinikia kitu chochote kile, uwe ni mwenge wa moto unaowaka au michirizi ya sauti ya ndege au miluzi inayotokana na upepo unapopeperusha matawi ya miti hali itakayoyaondolea masikio upweke usiojulikana. Watu wanataka utulivu lakini sio utulivu kupita kiasi. | Entry #22583 — Discuss 0 — Variant: Kenyan Winner
|
Kauli mbiu ya kizazi hiki, angalau katika ulimwengu ulioendelea, ni kuwa watu wanatamani kimya na hawakipati kabisa. Mngurumo wa trafiki, kukiriza kwa simu kusikokoma, matangazo ya kidijitali katika mabasi na magari moshi, kelele za runinga hata katika afisi zisizokuwa na watu, ni uvurugaji na mapigo yasiyokuwa na mwisho. Wanadamu wanajichosha kwa kelele na wanaishi kutamani kinyume chake -bila kujalisha kama ni mwituni, katika bahari iliyo wazi ama katika maeneo ya mapumziko fulani yaliyo na utulivu na umakinivu. Alain Corbin, Profesa wa Historia anaandika akiwa kambini katika eneo la Sorbonne na Erling Kagge, msafiri na mtafiti raia wa Norway kutokana na kumbukumbu zake za taka za bara la Antarctica ambako wote wawili wamejaribu kutoroka. Na ilhali wakati Bwana Corbin anaeleza katika ''A History of Silence'', kuna uwezekano mkubwa hakuna kelele nyingi kama ilivyokuwapo. Kabla tairi zilizokuwa zikiendeshwa kwa gesi na hewa, mitaa ya miji ilijaa kelele nyingi ya magurudumu yaliyotengenezwa kwa chuma na majembe ya farasi yaliyotengenezwa kwa mawe. Kabla ya rununu kupendelewa, mabasi na magari moshi yalijaa mazungumzo baina ya watu. Wauzaji wa magazeti hawakuacha tu bidhaa zao pamoja tu kwa unyamavu bali waliyatangaza magazeti yao kwa sauti za juu sawia na walivyofanya wauzaji wa cheri, violeti na samaki freshi. Sanaa ya uigizaji na michezo ya kuigiza yalijaa purukushani. Hata vijijini, wakulima wadogowadogo waliimba wakifanya kazi yao ngumu. Hawaiimbi siku hizi. Kilichobadilika hasa si sana kiwango cha kelele, ambazo karne za awali nazo pia zililalamika kuhusu, lakini kiwango cha usumbufu, unaochukua nafasi ambayo kimya chaweza kuteka. Kipo kitendawili kingine kinakuja, kwa kuwa kitakapoteka, ndani kabisa katika msitu wa misonobari , katika jangwa lililo wazi, katika chumba kilicho wazi kighafla -inaonesha ukosefu wa ujasiri zaidi ya kukaribishwa. Hofu huingia, sikio linakazika kwa chochote, bila kujalisha kama ni king'ora cha moto ama mwito wa ndege ama kelele za majani ya mti, vitaokoa dhidi ya utupu huu usiojulikana. Watu wanataka kimya, lakini sio hivyo sana. | Entry #22480 — Discuss 0 — Variant: Not specified Finalist
|
Gumzo kwa miaka mingi, hata katika ulimwengu ulioendelea, ni kwamba watu wanatamani ukimya na hawawezi kuupata. Muungurumo wa trafiki/foleni za magari, milio isiyokoma ya simu za mkononi, matangazo ya kidijitali katika mabasi na treni, TV zikiwaka hata katika ofisi tupu, ni mlolongo usiokwisha na kumvurugia mtu mawazo. Jamii ya binadamu inajichosha yenyewe kwa kelele na inatamani kinyume chake - iwe porini, au katika bahari pana au katika maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili ya kutulia na kukusanyikia. Alain Corbin, profesa wa historia, anaandika kutoka ukimbizini kwake huko Sorbonne, na Erling Kagge, mchunguzi wa Norway, toka katika kumbukumbu zake za taka za Antarctica, ambapo wote wamejaribu kukimbia. Na bado, kama Mr Corbin anavyoelezea katika "Historia ya Ukimya", labda hakuna kelele zaidi kuliko ilivyokuwa. Kabla ya matairi ya kujazwa upepo, barabara za jiji zilijaa kelele za kupasua masikio za magurudumu ya chuma na viatu vya farasi kwenye jiwe. Kabla ya kujitenga kwa hiari kwenye simu za mkononi, mabasi na treni zilijawa na mazungumzo. Wauza-magazeti hawakuacha vyombo vyao kimya, bali walitangaza kwa sauti ya juu, kama walivyofanya wauza matunda ya cheri, wauza mrujuani na wauza samaki wabichi aina ya bangala. Majumba ya tamthilia na maigizo yalikuwa ni vurugu za vilio na kuzomea. Hata mashambani, wakulima waliimba walipokuwa wakifanya kazi ngumu ya kuchosha. Hawaimbi siku hizi. Kilichobadilika sio kiasi cha kelele, ambazo karne zilizopita pia zililalamikia, bali kiasi cha kumvurugia mtu mawazo yake, ambacho kinachukua nafasi ambayo ukimya ungeweza kuchukua. Hapo linaonekana tatizo lingine kubwa, kwa sababu wakati kimya kinapoingia ndani ya kina cha msitu wa mipaini, katika jangwa tupu, katika chumba kilichoachwa wazi ghafla - mara nyingi huogopesha badala ya kukubalika. Hofu huingia ndani; sikio lenyewe hufunga kwa kitu chochote kile, kuvuma kwa moto au mwito wa ndege au mlio wa majani, kitu ambacho kitaliokoa sikio hilo kutokana na utupu huu usiojulikana. Watu wanataka ukimya, lakini sio kiasi hicho. | Entry #22328 — Discuss 0 — Variant: Tanzanian Finalist
|
Watu hutamani ukimya, bado hawatatizwi na ukimya huo, Mchumi Dhamira ya tangu zamani, angalau katika dunia iliyoendelea, ni kwamba watu hutamani ukimya lakini hawawezi wakaupata. Migurumo ya magari, mikwaruzo ya simu isiyokoma, matangazo ya kidijitari katika mabasi na magari ya moshi, kelele kubwa zitokazo kutoka kwa maruninga hata katika maofisi matupu, ni shambulio na vurugu zisizoisha. Jamii ya binadamu huwa inajichosha na kelele na hutamini kinyume chake- kama ni jangwani, katika maziwa mapana au katika faragha zilizotengwa ili kupata utulivu na umakinifu. Alain Corbin, profesa wa historia, anaandika kutoka kwa ngome yake kule Sorbonne, na Erling Kagge, mtafiti wa KiNorwe, kutoka kwa kumbukumbu zake za uharibifu wa Antarctica, ambako wote wawili wamejaribu kutoroka. Na bado, kama vile Bw Corbin anavyosema katika ''A History of silence'', kuna uwezekano kwamba hakuna kelele nyingi kama ilivyokuwa hapo mwanzoni.Kabla ya tairi hewa, mitaa katika miji ilikuwa imejaa mikwaruzo mikali ya magurudumu ya chuma na njumu kwa mawe. Kabla ya utengano wa kujitolea ulioletwa na simu tamba, mabasi na magari ya moshi yalikuwa yamejaa kelele za mazungumzo. Wauzaji wa magazeti hawakuziwacha bidhaa zao katika rundo tuli kama wamezipanga, bali walizitangaza kwa sauti ya juu, wachuuzu wa cheri, matundu ya urujuani and una safi walifanya hivyo hivyo. Vyumba vya maonyesho ya sanaa na opera vilikuwa vimejaa vurugu za kila aina. Vijijini pia, maskini waliimba huku wakifanya kazi za sulubu. Siku hizi hawaimbi. Kile ambacho kimebadilika sawa sio sana kiwango cha kelele, ambacho jamii za hapo awali zililalamikia, bali kiwango cha vurugu, ambacho kimechukua nafasi ambayo inaweza vamiwa na ukimya. Lakini sasa kuna kweli kinzani nyingine, kwa sababu unapovamia- kule ndani ya msitu wa msonobari, katika jangwa lililo wazi, katika chumba ambacho kimehamwa kwa haraka - mara nyingi huwa wa kuogofya badala ya kukaribishwa. Hofu hutanda: sikio nalo hutegwa ili linase chochote kile, kiwe ni sauti ya moto au mlio wa ndege au susuru ya majani, ambacho kitaliokoa kutokana na upweke huu usiodhihirika. Watu hupenda ukimya, lakini sio ukimya mwingi. | Entry #24179 — Discuss 0 — Variant: Not specified Finalist
|
Moja wa matamanio katika kizazi hiki, katika ulimwengu ulioendelea ni kuwa watu wanatamani kimya na hawakipati. Kelele ya magari, mlio wa simu, matangazo katika mabasi na treni, runinga zinazofanya kelele kwenye ofisi tupu ni vurugu isiyo na mwisho. Binadamu wanajichosha na kelele na wanatamani kinyume cha hali hii - ikiwa ni mbugani, kwenye bahari au kwenye maeneo yaliyotengwa kwa faragha na utulivu. Alain Corbin ambaye ni profesa wa historia anaandika akiwa Sorbonne. Nae Erling Kagge ambaye ni mchunguzi wa kutoka Norway anaandika kutoka kumbukumbu za Antaktika ambako wawili hawa walijaribu kutoroka. Hata hivyo Bwana Corbin anasema katika nakala yake ya "A History of Silence" - "Historia ya Kimya", pengine kiwango cha kelele hakijaongezeka kuliko hapo mbeleni. Kabla ya magurudumu, barabara zilijaa kelele za magurudumu ya chuma na miguu ya farasi kwenye barabara za mawe. Kabla ya mtu kujitenga kwa hiari akitumia simu ya mkononi, kelele kutokana na mazungumzo ndani ya mabasi na treni ilikuweko. Wachuuzi wa magazeti hawakuyaacha magazeti yajiuze, waliyanadi kwa sauti kubwa. Pia wauzaji wa matunda, maua na samaki waliokuwa tu wamevuliwa. Katika majumba ya sinema na michezo ya kuigiza kulikuwa na kelele nyingi. Hata kule mashambani wakulima waliimba wakifanya kazi ya sulubu. Siku hizi hawaimbi. Kilichobadilika sio kwa hali kubwa kiwango cha kelele ambacho katika karne zilizopita watu walilalamikia. Bali ni kiwango cha mambo yanayotuvuruga. Mambo haya yanachukua nafasi ya kimya. Kuna kinaya kingine kwasababu kinapovamia, katka msitu, jangwa, katika chumba tupu, kimya huwa na woga na hakikaribishwi. Uwoga huingia, masikio yanategwa kusikiza chochote. Iwe ni kelele ya moto, ndege wakiitana au minong'ono ya majani - haya yatanusuru kimya kutokana na utupu. Watu wanataka kimya, lakini kiasi tu. | Entry #23377 — Discuss 0 — Variant: Kenyan
|
Mada ya enzi, angalau katika ulimwengu ulioendelea, ni kwamba watu wanatamani sana unyamavu na hawaipati. Ngurumo ya vitu vya uchukuzi, miliyo ya simu isiyoisha, matangazo ya kitarakilishi kwenye mabasi na magari ya moshi, runinga zipigazo kelele hata kwenye maofisi yaliyo tupu, ni mashambulizi na makengeusho yasiyoisha. Jamii ya wanadamu yajichosha na kelele na yatamani kinyume chake—iwe porini, kwenye bahari kuu au pahali pa mapumziko iliyotengwa kwa utulivu na umakini. Alain Corbin, profesa wa historia, aandika kutoka katika kimbilio lake huko Sorbonne, na Erling Kagge, mvumbuzi wa kutoka Norway, kutoka katika kumbukumbu zake za taka za Antaktika, ambamo wote walijaribu kutorokea. Na bado, vile Bw Corbin anavyoonyesha kwenye "Historia ya Unyamavu", pengine hakuna kelele zaidi kuliko ilivyokuwa. Kabla ya magurudumu ya pumzi, barabara za jiji zilijaa kelele nyingi za magurudumu ya vyuma na viatu vya farasi kwenye mawe. Kabla ya matengano ya hiari kwenye simu za rununu, mabasi na magari ya moshi yalijaa mazungumzo. Wauzaji-magazeti hawakuwacha bidhaa zao kwenye rundo bubu, lakini walizitangaza kwa sauti ya juu, kama vile wachuuzi wa cheri, vayoleti na kibua safi. Sehemu za miigizo na muziki zilikuwa michafuko ya sauti zilizopazwa kwa kukubali au kutokubali. Hata mashambani, wakulima waliimba walipofanya kazi. Hawaimbi sasa. Kilichogeuka si kiwango cha kelele vile, ambacho karne zilizopita pia zililalamikia, lakini kiwango cha makengeusho, ambacho chachukuwa nafasi ambayo unyamavu ungevamia. Hapo kwaibuka ukweli kinza mwingine, kwa sababu inapovamia—katika kina cha msitu wa misonobari, kwenye jangwa lililo tupu, katika chumba kilochowachwa tupu kwa ghafla—mara nyingi huangaisha badala ya kuwa jambo la kukaribisha. Hofu huingia; sikio lakwamia chochote kisilika, iwe muunzi wa moto au mwito wa ndege au mchakacho wa matawi, ambacho kitakiokoa kutoka kwenye utupu huu usiojulikana. Watu wanataka unyamavu, lakini si kiasi hicho. | Entry #22475 — Discuss 0 — Variant: Kenyan
|
Maandhari ya umri, angalau katika ulimwengu ulioendelea, ni kwamba watu wanatamani kimya na hawawezi kupata. Sauti ya trafiki, simu za kutosha za simu za mkononi, matangazo ya digital katika mabasi na treni, TV inaweka hata katika ofisi zisizo na tupu, ni betri isiyo na mwisho na uharibifu. Jamii ya binadamu inajivunja yenyewe na kelele na inatamani kinyume chake-ikiwa katika pori, juu ya bahari pana au katika makao mengine ya kujitolea kwa utulivu na mkusanyiko. Alain Corbin, profesa wa historia, anaandika kutoka katika kukimbia kwake huko Sorbonne, na Erling Kagge, mchunguzi wa Norway, kutokana na kumbukumbu zake za taka za Antartika, ambapo wote wamejaribu kutoroka. Hata hivyo, kama Mr Corbin anasema katika "Historia ya Ukimya", labda hakuna kelele zaidi kuliko ilivyokuwa. Kabla ya matairi ya nyumatiki, barabara za jiji zilijaa magunia ya viziwi vya magurudumu ya chuma na farasi kwenye jiwe. Kabla ya kujitenga kwa hiari kwenye simu za mkononi, mabasi na treni zinaanza kwa mazungumzo. Wafanyabiashara wa gazeti hawakuacha bidhaa zao katika sehemu ya ukimya, lakini waliwaangaza kwa sauti ya kiasi cha juu, kama walivyofanya wachuuzi wa cherries, violets na mackerel safi. Ukumbi na opera walikuwa machafuko ya huzzahs na barracking. Hata katika mashambani, wakulima walisema walipokuwa wakipiga. Hawa imba sasa. Imebadilika sio kiasi cha kelele, ambazo karne zilizopita pia zililalamika, lakini kiwango cha kuvuruga, ambayo inachukua nafasi ambayo kimya inaweza kuathiri. Huko kuna kitambo kingine, kwa sababu wakati inapoingia-ndani ya kina cha msitu wa pine, katika jangwa la uchi, katika chumba cha ghafla kilichotoka-mara nyingi huathibitisha bila kukubalika. Hofu huingia ndani; sikio linaweka juu ya kitu chochote, kama moto-punda au ndege au wito wa majani, ambayo itauokoa kutokana na ukosefu huu usiojulikana. Watu wanataka kimya, lakini sio kiasi hichi. | Entry #23374 — Discuss 0 — Variant: Tanzanian
|
Kwa kiasi Fulani katika nchi zilizoendelea watu wana shauku ya kuwepo ukimya ambayo ni kauli mbiu ya muda mrefu lakini haupo. Mingurumo ya magari na watu, miito ya simu isiyoisha, matangazo yanayotolewa kwa njia ya kidijitali katika mabasi na garimoshi, pia sauti zinazopiga kelele za seti za televisheni katika maofisi matupu ni vitu vinavyotumika kufanya fujo na vurugu. Binadamu wanajichosha wenyewe kwa makelele kitu ambacho ni kinyume katika sehemu za mwituni, baharini au katika baadhi ya sehemu zilizohamwa na kutengwa kwa ajili ya utulivu na umakinifu. Profesa wa historia, Alain Corbin ameandika kuhusu kukimbilia kwake Sorbonne na kuhusu Erling Kagge ambaye ni raia wa Norway na mtafiti juu ya kumbukumbu zao za Antarctica ambako wote walijaribu kupakimbia. Kama ambavyo bwana Corbin ameeleza katika “Historia ya Ukimya”, inawezekana hakuna makelele zaidi kama ilivyokuwa. Kabla ya kuwepo matairi ya kujazwa upepo, mitaa ya mijini ilikuwa imejaa matairi ya vyuma na kwato za chuma za wanyama. Kabla ya utengaji wa hiari wa simu za mkononi, mabasi na garimoshi yalikuwa yakigubikwa na mazungumzo. Wauzaji wa magazeti hawakuziacha sehemu zao za biashara katika hali ya ukimya bali walizitangaza kwa sauti kubwa kama wafanyavyo wauzaji wa cheri, urujuani na samaki jamii ya bangala. Sehemu hizo ilikuwa imejaa makelele. Pia sehemu za vijijini, wakulima waliimba kama wafanyavyo watumishi wa nyumbani. Hivi sasa hawaimbi. Hivi sasa kilichobadilika siyo kiasi kingi cha kelele ambazo katika karne za nyuma zilikuwa zikilalamikiwa bali ni kiasi cha vurugu ambazo zimetawala katika sehemu ambazo zilitakiwa kuwa na utulivu. Kuna sura nyingine inaonekana kukinzana, kwa sababu hali hiyo inapokuwepo katika msitu mkubwa, jangwa kubwa, katika chumba ambacho kimehamwa ghafla mara nyingi inathibitisha usumbufu badala ya kufurahiwa. Hofu inatawala, masikio yanaathiriwa na vitu mbali mbali, ima mlipuko wa moto au mlio wa ndege au mtikisiko wa majani, hali hiyo itasaidiwa na hali ya ukimya. Watu wanahitaji ukimya ila siyo kwa kiwango hicho. | Entry #24217 — Discuss 0 — Variant: Not specified
|
Mada ya umri, angalau kwa kwa nchi zilizoendelea ambapo watu wanatamani utulivu na hawaupati.Mirindimo ya magari barabarani, miito isiyoisha ya simu za mkononi, matangazo ya kidigitali kwenye mabasi na garimoshi,Luninga zinazopiga kelele kwenye ofisi zisizo na watu ni wazimu usio na mwisho. Mashindano ya mwanadamu ni kujichosha mwenyewe na makelele na kusubiria kinyume chake, iwe porini , baharini au kwenye utulivu wa kuweza kufikiri. Alain Corbin ni profesa wa historia, aliandika akiwa ukimbizini huko Sorbonne,Erling Kagge ambaye ni mpelelezi wa kinorwei katika kumbukumbu zake katika ardhi ya Antarctica ambako walijaribu kutoroka. Kama bwana Corbin alivyobainisha katika "Historia ya Ukimya",inawezekana hakuna tena kelele kama ilivyokuwa awali. Kabla ya matairi hewa, mitaa ya jiji ilikuwa na magurudu ya chuma yasiyotoa kelele na viatu vya farasi juu ya mawe.Kabla ya kujitoa kwa hiari kwenye milio ya simu za mkononi , mabasi na garimoshi. Wauza magazeti hawakuuza magazeti kimya bali walitangaza tena kwa kupaza sauti ya juu kama wafanyavyo wachuuzi wa matunda kama cheri, urujuani na wachuuzi wa samaki.Jumba la maonyesho na maigizo lilijawa shangwe na zomea zomea.Sehemu za mashambani wakulima wanaimba huku wakifanya kazi ngumu. Siku hizi hawaimbi. Kilichobadilika siyo kiwango cha makelele, ambapo zama za kale walilalamikia pia, lakini tatizo ni kiwango cha wazimu au fadhaa ambacho kinatawala nafasi ambayo utulivu unaweza kuingilia.Kuna ukinzani unaojitokeza , kwasababu kimya kitakapovamia kwenye kina cha msitu, jangwaau chumba kilichowazi hali hiyo itafadhaisha au kuogofya. Nyemelea ndani kwa uwoga:masikio yapo tayari kusikia chochote iwe mlio wa moto au ndege au jani ambao utasaidia kuondoa huu ukimya.Watu wanahitaji utulivu lakini si kwa kiwango hiki. | Entry #22654 — Discuss 0 — Variant: Tanzanian
|
Mandhari ya umri, angalau katika ulimwengu ulioendelea, ni kwamba watu wanatamani kimya na hawawezi kupata. Sauti ya trafiki, simu za kutosha za simu za mkononi, matangazo ya digital katika mabasi na treni, TV inaweka hata katika ofisi zisizo na tupu, ni betri isiyo na mwisho na uharibifu. Jamii ya binadamu inajivunja yenyewe na kelele na inatamani kinyume chake-ikiwa katika pori, juu ya bahari pana au katika makao mengine ya kujitolea kwa utulivu na mkusanyiko. Alain Corbin, profesa wa historia, anaandika kutoka katika kukimbia kwake huko Sorbonne, na Erling Kagge, mchunguzi wa Norway, kutokana na kumbukumbu zake za taka za Antarctica, ambapo wote wamejaribu kutoroka. Hata hivyo, kama Mr Corbin anasema katika "A History of Silence", labda hakuna kelele zaidi kuliko ilivyokuwa. Kabla ya matairi ya nyumatiki, barabara za jiji zilijaa magunia ya viziwi vya magurudumu ya chuma na farasi kwenye jiwe. Kabla ya kujitenga kwa hiari kwenye simu za mkononi, mabasi na treni zinaanza kwa mazungumzo. Wafanyabiashara wa gazeti hawakuacha bidhaa zao katika rundo la mute, lakini waliwaangaza kwa kiasi cha juu, kama walivyofanya wachuuzi wa cherries, violets na mackerel safi. Theater na opera walikuwa machafuko ya furaha. Hata katika mashambani, wakulima walisema walipokuwa wakipiga. Hawana kuimba sasa. Imebadilika sio kiasi cha kelele, ambazo karne zilizopita pia zililalamika, lakini kiwango cha kuvuruga, ambayo inachukua nafasi ambayo kimya inaweza kuathiri. Huko kuna kitambo kingine, kwa sababu wakati inapoingia-ndani ya kina cha msitu wa pine, katika jangwa la uchi, katika chumba cha ghafla kilichotoka-mara nyingi huathibitisha bila kukubalika. Hofu huingia ndani; sikio linaweka juu ya kitu chochote, kama moto-punda au ndege au wito wa majani, ambayo itauokoa kutokana na ukosefu huu usiojulikana. Watu wanataka kimya, lakini sio kiasi. | Entry #23078 — Discuss 0 — Variant: Not specified
|